Juan Martin kwa mara nyingine akatisha ndoto za Federer kukutana na Nadal Us Open
Katika vitu mashabiki wengi wa mchezo wa tennis walikuwa wakikisubiria kwa hamu baasi ilikuwa kuwaona wababe wawili wa mchezo huo Rafael Nadal na Rodger Federer kukutana katika Us Open.
Lakini Juan Martin Del Potro amekatisha ndoto hiyo ya wapenzi wa tennis baada ya kumfunga na kumuondoa Rodger Federer kwa kumpiga seti 7-5,3-6,7-6 na 6-4 katika mchezo ambao Federer alipewa nafasi kubwa kuibuka kidedea.
Kama Federer angeshinda mchezo huu dhidi ya Martin Del Potro baasi angeenda kupambana na Nadal lakini tofauti na matamanio ya wengi sasa Del Potro ndio anakwenda kukutana na Rafael Nadal.
Del Potro anaonekana amekuwa kizuizi kikubwa kwa wafalme hawa kukutana kwanu miaka nane iliyopita alimtoa Nadal katika mashindano haya na kisha akaenda katika fainali na kumfunga Rodger Federer.
Kwa matokeo haya sasa Del Potro anakwenda kukutana na Rafael Nadal siku ya Ijumaa katika fainali ya michuano hii huku Nadal akipewa nafasi kubwa kulipiza kisasi kwa Potro kwa matokeo yaliyotokea miaka 8 iliyopita.
0 comments:
Post a Comment