Kwa rekodi hii ya Mayanga, Stars itafika tunapotaka?
January 4, 2017 TFF ilimtangaza Salum Mayanga kuwa kocha wa Taifa Stars akichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa aliyekuwa mtangulizi wake.
Hadi sasa Mayanga amejiwekea rekodi nzuri akiwa kocha wa Stars. Ameisimamia katika mechi 12, ameshinda mechi sita, sare tano na kupoteza mechi moja.
Mayanga aliiongoza Stars kumaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA 2017 iliyofanyika Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Juni hadi mwanzoni mwa July.
Reko ya Salum Mayanga katika mechi 12 alizoiongoza Stars kama kocha mkuu
25/03/2017 Tanzania 2-0 Botswana (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
28/03/2017 Tanzania 2-1 Burundi (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
10/06/2017 Tanzania 1-1 Lesotho (kufuzu AFCON)
25/06/2017 Tanzania 2-0 Malawi (COSAFA)
27/06/2017 Angola 0-0 Tanzania (COSAFA)
29/06/2017 Tanzania 1-1 Mauritius (COSAFA)
02/07/2017 Afrika Kusini 0-1 Tanzania (COSAFA)
05/07/2017 Zambia 4-2 Tanzania (COSAFA)
07/07/2017 Tanzania 0-0 Lesotho (Stars ilishinda kwa penati 4-2 COSAFA)
15/07/2017 Tanzania 1-1 Rwanda (kufuzu CHAN)
22/07/2017 Rwanda 0-0 Tanzania (kufuzu CHAN)
02/09/2017 Tanzania 2-0 Botswana (mechi ya kirafiki ya kimataifa)
Kutokana na rekodi hiyo aliyonayo Mayanga, kuna haja ya kutafuta kocha mpya wa kuifundisha Stars? Nipe maoni yako kwa kuniandikia comment yako hapo chini
0 comments:
Post a Comment