Kesho Jumamosi ya September 9, 2017 ligi kuu Tanzania bara
itaendelea kwa mechi kadhaa kuchezwa kwenye viwanja mbalimbali, mechi
kubwa jijini Dar ni kati ya Azam FC vs Simba mechi ambayo huitwa derby
ndogo pindi Azam inapocheza na Simba au Yanga.
Mechi ya Azam vs Simba ndio itafuatiwa na mashabiki wengi wa soka Tanzania kati ya mechi zitakazochezwa Jumamosi hii, ni mechi yenye vitu vingi ndani yake lakini shaffihdauda.co.tz imeamua kumuka mambo haya.
Azam vs Simba kwa mara ya kwanza Azam Complex
Tangu Azam imeanza kumiliki uwanja wake wa nyumbani Azam Complex imekuwa ikiutumia uwanja huo kwa mechi zao zote za kimataifa huku mechi za ligi zikiwa ni dhidi ya timu nyingine na si Simba wala Yanga.
Mechi zote za nyumbani za Azam dhidi ya Simba na Yanga zimekuwa zikichezwa kwenye uwanja wa Taifa au Uhuru kwa visingizio kwamba uwanja wa Azam Complex ni mdogo hauwezi kumudu idadi ya mashabiki wa timu hizo mbili na matokeo yake usalama utakuwa ni mdogo.
Safari hii Azam itacheza kwa mara ya kwanza mechi zake zote kwenye uwanja wao wa nyumbani ikiwemo za Simba na Yanga baada ya bodi ya ligi kuamua Simba na Yanga zikacheze Azam Complex.
Manula, Nyoni, Bocco na Kapombe watapambana kuiua timu yao ya zamani
Aishi Manula, Erasto Nyoni, John Bocco na Shomari Kapombe ni wachezaji waliocheza Azam FC kabla ya kuondoka baada ya msimu uliopita kumalizika. Wote kwa pamoja wamesajiliwa na Simba, watakuwa wakirejea Azam Complex wakiwa wapinzani.
Manula na Nyoni watakuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Simba kitakachoikabili Azam, Bocco huenda akaingia kama mwalimu ataamua kumchezesha lakini Kapombe ataukosa mchezo huo kutokana na majeraha ya muda mrefu yanayomsumbua.
Rekodi ya Simba vs Azam kwa mechi 6 zilizopita
Katika mechi sita za ligi zilizopita timu hizi kukutana, Simba imeshinda mara mbili Azam imeshinda mechi mechi moja halafu mechi tatu nyingine timu hizo zimetoka sare.
09/09/2017 Azam ?? Simba
28/01/2017 Simba 0-1 Azam
17/09/2016 Azam 0-1 Simba
01/05/2016 Simba 0-0 Azam
12/12/2015 Azam 2-2 Simba
02/05/2015 Simba 2-1 Azam
24/01/2014 Azam 1-1 Simba

0 comments:
Post a Comment