Kuelekea mchezo wa Azam V Simba: Haya ndio Mambo 7 muhimu kuhusu John Bocco na soka
Ni mmoja wa washambuliaji bora katika kizazi cha sasa cha soka. Amecheza katika ligi kuu ya Tanzania bara kuanzia msimu wa 2008/09 kwa mafanikio makubwa akiwa nahodha wa klabu ya Azam, ambayo ameitumikia mpaka msimu uliopita kabla ya msimu huu kuelekea mtaa wa Msimbazi.
Jumamosi hii huenda akawa miongoni mwa wachezaji 22 watakaounda kikosi cha Simba kitakachoenda Chamazi Complex kuumana na Azam FC. Siku kadhaa zilizopita nilipata nafasi ya kumuuliza John Bocco maswali 7 muhimu kuhusu soka na career yake kiujumla;
1: Nilijua ningefanikiwa kama mwanasoka……
“Mara tu nilipojiunga na Azam FC kutokea Cosmopolitan. Tofauti na timu nyingine za kitanzania, niliona Azam wakiwa na mipango thabiti na endelevu katika kuendeleza kipaji changu as a footballer. Pia ujio wa Maximo nchini na falsafa yake ya kuamini vijana ulinipa moyo kwamba ningefanya jitihada ningefanikiwa zaidi.
2: Siku yangu ya furaha zaidi kwenye soka….
Ilikuwa siku nilipoifungia timu yangu ya Azam FC magoli mawili yaliyoipandisha daraja – kutoka daraja la kwanza mpaka ligi kuu. Sitoisahau hiyo siku.
3: Kama ningepata nafasi ya kubadili kitu kimoja katika soka……………..
Kuondoa mfumo mbovu uliopo sehemu kubwa katika ukuzaji wa vipaji. Academy bora na zenye malengo ndio mwokozi wa soka letu, tuwekeze kwenye soka na baadae tutaona faida yake.
4: Maneno matatu yanayonielezea vizuri ni…………………
Mpole, mstaraabu na mfanyakazi kwa bidii.
5: Kama nisingecheza soka….
Sijawahi kufikiria kufanya shghuli nyingine yoyote kabla ya soka, wakati naanza kupata ufahamu siku zote nilikuwa nataka nifanikiwe kwenye soka kama staa wetu wa kipindi kile Edibily Jonas Lunyamila.
6: Shujaa wangu kwenye soka ni…
Edibily Jonas Lunyamila, huyu ndio idol wangu.
7: Siku ya huzuni kwenye maisha yangu ya kisoka ukiwa na Azam FC..
Siku tulipofungwa na Yanga kwenye fainali yetu ya kwanza ya Kagame Cup mwaka 2012.
0 comments:
Post a Comment