Tuesday, September 5, 2017

Mario Gomez akishangilia baada ya kuifungia bao la sita Ujerumani dakika ya 79 katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Norway jana kwenye mchezo wa Kundi C kufuzu Kombe la Dunia mwakani Urusi uliofanyika Uwanja wa Mercedes-Benz-Arena mjini Stuttgart. Mabao mengine ya Ujerumani yalifungwa na Mesut Ozil dakika ya 10, Julian Draxler dakika ya 17, Timo Werner mawili dakika za 21 na 40 na Leon Goretzka dakika ya 50

0 comments:

Post a Comment