Wednesday, November 29, 2017


Mashabiki wengi wa Barcelona walisikitika sana baada ya Neymar kuwaacha na kujiunga na PSG, Neymar alikuwa mchezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Barcelona lakini Lioneil Messi ana mawazo tofauti.
Lioneil Messi yeye anaona kuondoka kwa Neymar kumewafanya Barcelona wacheze vizuri zaidi haswa eneo lao la ulinzi, Messi anaamini tangu Neymar aondoke safu yao ya ulinzi imekuwa imara zaidi.
Tangu Neymar aondoke, kocha wa klabu ya Barcelona Ernesto Valverde amebadili mfumo toka ule uliowafanya MSN kufunga mabao 364 katika miaka mitatu (4-3-3) hadi kuwapeleka katika mfumo mama wa 4-4-2.
Lioneil Messi anaamini katika safu yao ya ushambuliaji kuna kitu kimepungua kutokana na kuondoka kwa Neymar lakini timu yao imekuwa na balance nzuri zaidi kati ya ushambuliaji na uzuiaji.
Kuhusu timu tishio kwao msimu huu Messi anaamini Man City ni tishio kubwa sana barani Ulaya safari hii na pia PSG, lakini akasisitiza kwamba Real Madrid ni timu kubwa kwahiyo nayo isichukuliwe poa.

0 comments:

Post a Comment