Wednesday, November 29, 2017

Grigory Rodchenkov amewahi kufanya kazi kwenye kitengo cha kupambana na dawa hizo


Mpelelezi wa Urusi Grigory Rodchenkov anatuhimiwa na shirika la kupambana na dawa zilizokataliwa michezoni duniani (WADA) kwa kugawa dawa hizo kwa wanariadha wa Urusi.
Serikali ya Urusi imesema kwamba wanariadha wake hawakujua kuwa Grigory Rodchenkov alikuwa akiwapa dawa ambazo zinaongeza nguvu.
Rodchenkov amewahi kuwa mkuu wa kitengo cha kuzuia dawa hizo mjini Moscow.
Tuhuma hizi zinakuja siku chache baada ya wanariadha wa Urusi kufungiwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Olimpiki mwaka 2018 yatakayofanyika Koreka Kusini.
Awali WADA imewahi kumshutumu Rodchenkov kwa kuharibu sampuli za wanamichezo wa Urusi maksudi ili kuondoa ushahidi.

0 comments:

Post a Comment