Tuesday, November 28, 2017



Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Real Madrid, AC Milan, Man City na sasa anaichezea Atletico Mineiro ya kwao Brazil Robson De Souza maarufu kama Robinho, leo Alhamisi ya November 23 2017 amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela.

Robinho amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela kwa kuwa miongoni mwa kundi la watu watano waliyohusika na kumdhalilisha msichana raia wa AlbaniaJanuary 22 2013 nchini Italia katika jiji la Milan, wakati huo Robinho na washikaji zake walikuwa Night Club.

Wakati Robinho anatenda kosa hilo alikuwa akiichezea club ya AC Milan ya Italia lakini anayo nafasi ya kukata rufaa na kwa mujibu wa sheria za Italia Robinho kama atakata rufaa hatofungwa hadi rufaa yake isikilizwe kitu ambacho kinaweza kikachukua miaka mingi rufaa hiyo kusikilizwa.

VIDEO: Yanga ilivyoiadhibu Mbeya City leo Chirwa akipiga hat-trick Nov 19 2017

0 comments:

Post a Comment