Wednesday, November 29, 2017


Fury baada ya kumchapa Wladimir Klitschko mwaka 2015
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu duniani Tyson Fury amesema atapenda kupigana na mtu mwenye jina kubwa iwapo atarejea uwajani.
Fury mwenye miaka 29 tiyari ameshasaini mkataba na kampuni ya MTK akijiandaa kumaliza adhabu yake.
Anatarajia kusikia uamuzi wa mahakama mwezi Desemba dhidi ya kesi yake ya matumizi ya dawa zilizokataliwa michezoni mwaka 2016.
''Naweza kuitwa mkorofi, mgomvi na mambo mengine ya aina hiyo, lakini sio mtumizi wa dawa za kuongeza nguvu,'' alisema Fury raia wa Uingereza.
Chama cha ndondi nchini Uingereza kimesema bingwa huyo ambaye alipata mikanda ya IBF, WBA na WBO kwa kumchapa Wladimir Klitschko Novemba 2015, hatopewa leseni ya kupigana mpaka pale mambo yote yatakapowekwa sawa.

0 comments:

Post a Comment