Wednesday, December 20, 2017

Sakata la mchezaji Asante Kwasi anayetajwa kusajiliwa na klabu ya Simba lakini hadi sasa klabu ya Lipuli haijui mchezaji huyo yupo wapi. Uongozi wa Lipuli umesema unasubiri maelezo kutoka kwa Kwasi juu ya kuchelewa kujiunga na kambi baada ya ruhusa aliyopewa kumalizika lakini bado hajarejea na hakuna taarifa yoyote aliyotoa kwa uongozi wake.
Mwenyekiti wa Lipuli Ramadhani Mahano ametoa sababu kadhaa akieleza kwa nini Lipuli inasema Kwasi ni mchezaji wao halali.
“Tuliingia mkataba na Kwasi Julay 30, 2017 tuna mkataba wa mwaka mmoja, mkataba  wake unaisha Julay 29, 2018. Kwa maana hiyo inaonesha kwamba Simba watakuwa wamekiuka vipengele vingi vya usajili, ieleweke kwamba mchezaji yoyote ambaye bado anamkataba wa zaidi ya miezi sita na klabu yake kanuni za TFF na FIFA haziruhusu mchezaji huyo kuongea na klabu yoyote juu ya usajili.”
“Singida waliandika barua lakini walitoa ofa ya shilingi 10 miloni kwa sababu ofa yao ilikuwa chini sana tulishindwa hata kuwajibu kwa hiyo tukawa tunawasikiliza kama wataongeza ofa yao ili tuweze kufanya mazungumzo. Sisi tulihitaji juu ya hapo ili aweze kuondoka na kwenda kuitumikia klabu yoyote.”
“Bado hatujakutana kamati ya utendaji kwa sababu tunapenda kukaa pamoja na kukaa pamoja, kwa hiyo tutasikiliza kama kuna klabu itakuja au kuonesha nia ya kumchukua tutakaa chini na kupanga tutamtoa Kwasi kwa kiasi gani cha pesa.”
“Baada ya kusikia tetesi zote hizo, mnamo December 12, 2017 klabu ya Lipuli tuliandika barua TFF tukitoa angalizo kwa vilabu vyote ambavyo vinajaribu kurubuni wachezaji wetu akiwemo Asante Kwasi juu ya kusajiliwa na klabu yoyote.”
“Hakuna klabu yoyote iliyokuja hadi sasa kwa ajili ya mazungumzo ya kumsajili Kwasi kwa hiyo, sisi klabu ya Lipuli hatuna la ziada isipokuwa tunasubiri TFF ibandike majina ya wachezaji wote waliosajiliwa baada ya dirisha dogo kufungwa na watangaze muda wa pingamizi ambapo sisi tutapinga usajili wowote ambao utakuwa umefanywa ukimuhusisha mchezaji huyo. Barua tuliyoiandikia TFF itakuwa ushahidi na tutakuwa tayari kwenda kuonesha vielelezo vyetu vinavyotufanya tuseme Kwasi ni mchezaji wetu halali.”
Inaelezwa kwamba, baada ya mchezo wa Simba dhidi ya Lipuli Kwasi alipewa ruhusa ya wiki mbili kwenda nyumbani kwao Ghana kuhudhuria mazishi ya baba yake baadae aliomba mshara wake na nauli ya kwa ajili ya kurudi nchini akatumiwa na uongozi wa klabu yake na wakawa wanatarajia atawasili Iringa December 16, 2017.
Tayari ruhusa yake imemalizika lakini Kwasi bado hajaripoti Lipuli hivyo uongozi wa klabu hiyo umepanga umepanga kumpa onyo kwa sasababu yupo nje ya tarehe ambayo alipangiwa kurejea kwenye klabu yake.

0 comments:

Post a Comment