WAKATI sakata la uwekezaji
likiendelea kuteka hisia za wadau wengi wa soka la nchini Tanzania,
hatimaye serikali imetoa tamko juu ya aina ya uwekezaji ambao unatakiwa
na ulioruhusiwa.
Hivi karibuni kuliibuka juu ya
maamuzi ya uwekezaji ambapo Klabu ya Simba ilikuwa kwenye mchakato wa
kufanya mabadiliko ya umiliki na uongozi wa klabu kama ilivyo kwa Yanga.
Inalezwa kuwa mwanachama wa Simba,
Mohamed Dewji ‘Mo’ anawania nafasi ya kumiliki hisa pindi mabadiliko
yatakapofanyika, huku Yanga mtu aliyekuwa akitajwa ni mfanyabiashara
Yusuf Manji ambaye alikuwa mwenyekiti wa klabu hiyo.
Akizungumza kwa ufupi kuhusu suala
hilo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison
Mwakyembe ametamka kuwa wao serikali wameruhusu uwekezaji na wapo tayari
kuona hilo likifanyika.
Amesema pamoja na kukubaliwa
lakini mwekezaji mkuu anatakiwa kumiliki hisa zisizozidi asilimia 49 ili
kuwapa nafasi wale wamiliki halisi wa klabu kuendelea kuwa na sauti.
Ameongeza kuwa serikali haikatazi
uwekezaji lakini hilo linaweza kufanyika kwa kuzingatia kigezo hicho ili
kutoondoa umiliki wa klabu hasa zile za wanachama.
Ametolea mfano nchini Ujerumani
ambapo mfumo huo unatumika na umekuwa na msaada katika kukuza soka la
ndani la nchi hiyo tofauti na Uingereza ambapo mwenye fedha nyingi
anamiliki klabu na ndiye anakuwa na sauti.
0 comments:
Post a Comment