Meneja wa Arsenal,
Arsene Wenger anahofia mshambuliaji Alexandre Lacazette ''hatakuwa
uwanjani kwa muda'' baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu siku ya
Jumatano, katika mecho ambayo walipata ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya
Huddersfield.
Lacazette, 26, alifunga bao la kwanza lakini alitolewa uwanjani wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Oliver Giroud.Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amefunga magoli saba kwa Gunners tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Lyon mwezi Julai kwa kitita cha £46.5m.
''Ni bayana hatashiriki mechi ya wikendi hii,'' Wenger amesema.
''Alipata jeraha kwenye kifundo cha mguu wake. Atakuwa nje ya mchezo kwa muda.''
0 comments:
Post a Comment