Friday, December 1, 2017

Sam Allardyce (katikati) alionekana na mmiliki wa Everton Farhad Moshiri katika uwanja wa Goodison Park siku ya Jumatano


Klabu ya soka ya Everton ya Uingereza imempa kibarua cha kuinoa klabu hiyo meneja Sam Allardyce.
Allardyce amesema ana furaha na faraja kujiunga na klabu ya Everton.
Big Sam mwenye miaka 63 kocha wa zamani wa timu ya taifa ya England amesaini mkataba utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2019 akichukua mikoba ya Ronald Koeman aliyetimuliwa mwezi Oktoba baada ya timu hiyo kuanza ligi vibaya.
Allardyce amekuwa nje ya uwanja tokea alipoachana na klabu ya Crystal Palace mwezi Mei.
Ni mashuhuri sana kwa kuzisaidia timu ambazo zinakaribia kushuka daraja zisailie kwenye EPL

0 comments:

Post a Comment