Muingereza Gordon
Reid ameshinda mchezo wake wa pili katika mashindano ya walemavu ya
Tennis Masters na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia kwenye hatua
ya nusu fainali itakayopigwa mjini Loughborough.
Baada ya kupoteza
mbele ya bingwa Joachim Gerard siku ya Jumatano, Reid amemshinda
Nicolas Peifer wa Ufaranda kwa seti 3-6 6-4 6-3.Muingereza mwenzake Andy Lapthorne nae pia amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumchapa Heath Davidson wa Australia kwa seti 6-2 7-5.
Alfie Hewett naLucy Shuker walipoteza michezo yao.
Hewett, namba mbili kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume, alipangwa kucheza na Shingo Kunieda wa Japan lakini alipoteza kwa seti 2-6 6-4 6-2 baada ya kuumia bega.
0 comments:
Post a Comment