Saturday, January 13, 2018


Mashabiki wa Arsenal wamekuwa na kilio cha muda mrefu kuhusu kocha wao mkuu Arsene Wenger, mashabiki wengi wamekuwa wakitaka Arsene Wenger kuachana na klabu yao kwani wanamuona kama kikwazo.
Mzee Wenger anaonekana kama tatizo katika klabu ya Arsenal kutokana na kushindwa kuendana na kasi ya makocha wa kizazi kipya cha soka ambao wamejazana EPL kama Antonio Conte na Jose Mourinho.
Kwa mara nyingine tena Arsene Wenger amezungumzia mustakabali wake ndani ya Arsenal, Wenger amesisitiza kwamba haondoki ng’o katika klabu hiyo na yupo hata msimu ujao wa ligi ya EPL.
Arsene Wenger amesema ataendelea kufanya maamuzi sahihi ya kuisaidia klabu hiyo kama alivyokuwa akifanya mwanzo huku pia akithibitisha kwamba Alexis Sanchez ataondoka katika klabu hiyo mwezi huu.
Wiki hii kulikuwa na tetesi kwamba kocha Carlo Ancelotti ameanza mazungumzo kusaini mkataba wa awali na Arsenal ambapo alitarajiwa kuanza kuinoa msimu ujao wa ligi lakini sasa inaonekana suala hilo ni gumu kutokea.

0 comments:

Post a Comment