Kipindi kigumu cha
Arsenal kiliendelea baada ya mabao kutoka kwa Callum Wilson na Jordon
Ibe kuiwezesha Bournemouth kutoka nyuma na kuwashinda kwa mabao 2-1.
Sasa
kikosi cha Arsene Wenge kina mechi tano bila ushindi na kubaki nyumba
kwa pointi tano wakati Bournemoutha wakiendelea na mechi nne bila ya
kushindwa.Mlinzi Hector Bellerin aliwapatia wageni waliocheza bila ya Alexis Sanchez, uongozi wakati Alex Iwobi alipomimina kombora kumzidi Asmir Begovic.
Lakini Wilson alitumia fusra ya makosa yake Petr Cech na kutumbukiza mpira wavuni.
Upande wa Eddie Howe ulipata ushindi wa kwanza kabisa dhidi ya Arsenal na kupanda hadi nafasi ya 13 na pointi 4 kutoka hatarini.
0 comments:
Post a Comment