Baada ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa Bournemouth, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akafunguka kuwa hatma ya Alexis Sanchez imewadia.
Ingawa Wenger hakutaka kuweka wazi ni wapi mchezaji huyo anaelekea lakini alisema: "Sijausoma vizuri huu mwendo ila inaweza kutokea leo, au kesho au isitokee, itajulikana saa 48 zijazo."
Sanchez hakusafiri na timu kwenda kuikabili Bournemouth
na Wenger alipoulizwa iwapo hatua hiyo inaashiria kuondoka kwa Sanchez
akasema: "Ndiyo. Usizame sana kwenye hili kwasababu hata mimi sijajua
ni kwa namna gani itafanyika".
Manchester
United wanaongoza mbio za kuwania saini ya Sanchez mbele ya Manchester
City ingawa Liverpool nayo inatajwa kuwa inatajwa kuwemo kwenye mbio
hizo.
Mwandishi maarufu wa Italia Gianluca Di Marzio anadai tayari Manchester United imekubaliana na Sanchez juu ya maslahi yake binafsi.
0 comments:
Post a Comment