Nyota Mnigeria, Kelechi Iheanacho (kulia) akishangilia baada ya kuifungia mabao yote mawili Leicester City dakika za 43 na 77 ikishinda 2-0 dhidi ya Fleetwood
ya Daraja la Kwanza katika mchezo wa Kombe la FA jana Uwanja wa King
Power, Leicester. Hata hivyo, kwa bao la pili ilibidi kwanza refa Jon
Moss athibitishiwe kupitia teknolojia ya picha za video (VAR) kwamba
Iheanacho hakuwa ameotea baada ya awali kukataliwa akidhaniwa alikuwa
ameotea. Iheanacho anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza England bao
lake kuhalalishwa na mfumo wa VAR baada ya awali kukataliwa kwa
kudhaniwa ameotea
Home
»
»Unlabelled
» IHEANACHO AFUNGA YOTE LEICESTER CITY YASHINDA 2-0 KOMBE LA FA
Wednesday, January 17, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment