Wednesday, January 17, 2018


Alianza na Gremio na huko namba zinaonesha kwamba Ronaldinho alicheza michezo 145 na kati ya hiyo alifunga mabao 72 kabla ya kwenda PSG ambako alifunga mabao 25 kwenye mechi 86.
Alipofika Barcelona ndio mambo yalizidi kuwa moto zaidi kwani Dinho alifanikiwa kucheka na nyavu mara 97 katika michezo 207 kabla ya kwenda Ac Millan akicheza mechi 95 na kufunga mabao 26.
Maisha ya Ronaldinho yalianza kuyumba aliporudi Atletico Mineiro ambapo michezo 85 alifunga mabao 27, Quretatro alifanikiwa kufunga mabao 8 tu katika mechi 8 lakini Fluminese hakufunga bao hata moja katika mechi 0.
Timu ya taifa ya Brazil nako Ronaldinho Gaucho alifanikiwa kuitumikia michezo 97 ambako katika michezo hiyo Mbrazil huyo aliifungia timu ya taifa mabao 33 akishinda kombe la dunia pia.

0 comments:

Post a Comment