BAO
pekee la Junior Makiesse dakika ya 73 limeipa ushindi wa 1-0 Kongo
dhidi ya Cameroon katika mchezo wa Kundi D michuano ya Ubingwa wa
Mataifa ya Afrika (CHAN) inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za
nchini mwao mjini Agadir jana.
Simba Wasiofungika walio chini ya kocha, gwiji wa Cameroon, Rigobert Song walitawala mchezo, lakini wakashindwa kutawala mahesabu ingawa walitengeneza nafasi kadhaa.
Patrick Moukoko wa Cameroon alikosa bao dakika tatu kabla ya mapumziko akiwa umbali wa mita sita baada ya shambulizi zuri kutoka upande wa kulia ambako Thomas Bawak na Junior Awono waligongeana vizuri.
Kongo sasa inapanda kileleni mwa Kundi D, baada ya Angola na Burkina Faso kumaliza mechi yao kwa sare ya 0-0 jana jioni.
CHAN inaendelea leo kwa mechi za Kundi A; wenyeji, Morocco wakimenyana na Guinea Saa 1:30 usiku, kabla ya Sudan kuvaana na Mauritania Saa 4: 30 usiku.

0 comments:
Post a Comment