Wednesday, January 17, 2018


Ronaldo De Assis Moreira “Gaucho” alizaliwa mwaka 1980 katika mji wa Porto Alegre mjini Brazil ambako tangu akiwa na miaka 7 tayari alianza kuwa gumzo katika mtaa wao kutokana na uwezo wake.
Kama ilivyo kwa wanasoka wengine wa Kibrazil, Ronaldinho Gaucho naye alianza soka lake kwa kucheza samba mtaani kwao Brazil baadaye akaonekana na kupelekwa katika klabu ya Gremio alikoanza kuvaa viatu.
Mwaka 2001 klabu ya Paris Saint German walimuona Gaucho na wakamchukua na mwaka 2003 alihamia Nou Camp kwenda kukipiga Barcelona na hapo ndio dunia nzima ilianza kumjua Gaucho.
Barcelona ndipo ambapo Ronaldinho alishinda karibia kila kitu, alibeba makombe mawili ya ligi, akaja akabeba Ballon D’or mwaka 2006 lakini vile vile akabeba kombe la Champions League mwaka 2006.
Baada ya Frank Rijkaard kuiacha Barcelona na kuja Pepe Gurdiola aliamja kumuuza Ronaldinho kwenda Ac Millan ambako ilishuhudiwa wakibeba kombe la Serie A msimj wa 2010/2011 na msimu huo huo Ronaldinho akatoswa timu ya taifa.
Baada ya Ronaldinho kuondoka Ac Millan ndipo mambo yalianza kuwa magumu akarudi nchini kwao Brazil kuitumikia Flamengo, Atletico Mineiro na Fluminesse ambako ndiko alikostaafia soka.

0 comments:

Post a Comment