Saturday, January 13, 2018

Fousseni Diabate kutoka Mali


Leicester imemsajili mshambuliaji wa Mali Fousseni Diabate kutoka klabu ya ligi ya daraja la pili nchini Ufaransa Gazelec Ajaccio kwa dau lisilojulikana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ametia saini kandarasi ya miaka minne na nusu na klabu hiyo ya Uingereza.
Akiwa kinda wa chuo cha soka cha Stade Rennais , anaweza kucheza kama winga ama hata mshambuliaji na ameichezea klabu yake mara 20.
Diabate ameiwakilisha Mali katika soka ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 na 23.

0 comments:

Post a Comment