Monday, January 15, 2018

Mshambuliaji Msenegali, Sadio Mane akikimbia kushangilia na beki wa kushoto, Andy Robertson baada ya kuifungia Liverpool bao la tatu dakika ya 61 katika ushindi wa 4-3 dhidi ya Manchester City leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield. Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya tisa, Roberto Firmino dakika ya 59 na Mohamed Salah dakika ya 68, wakati ya Man City inayopoteza mechi ya kwanza msimu huu yamefungwa na Leroy Sane dakika ya 40, Bernardo Silva dakika ya 84 na Ilkay Gundogan dakika ya 90 na ushei

0 comments:

Post a Comment