Zimetimia mechi saba sasa Mbeya City imeshindwa kupata ushindi mbele ya Tanzania Prisons kwenye michezo ya ligi kuu tanzania bara baada ya mbeya city kujikuta ikipoteza mchezo wa leo wa ‘Mbeya derby’ dhidi ya Prisons kwa mabao 3-2 kwenye uwanja wa sokoine ndani ya Green City.
Timu hizo zimekutana leo Januari 14, 2017 ikiwa ni mchezo wa tisa (9) tangu Mbeya City ipande daraja kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu wa 2013/14. Ushindi wa mwisho wa mbeya city dhidi ya tanzania prisons ulikuwa 30/03/2014 waliposhinda 1-0.
Katika mechi tisa ambazo Mbeya City na Tanzania Prisons zimekutana kwenye ligi, Mbeya City imeshinda michezo miwili pekee ilishinda mechi zote mbili za msimu wake wa kwanza ikiwa chini ya kocha Juma Mwambusi. Prisons yenyewe imeshinda mechi nne huku michezo mitatu timu hizo zikitoka sare.
Ushindi wa leo wa Tanzania Prisons ni wa pili mfululizo dhidi ya Mbeya City, Prisons walitangulia kupata goli la kuongoza dakika ya 8 likifungwa na Salum Bosco lakini Mbeya City wakasawazisha dakika ya 30 kupitia kwa John Kibanda. Prisons wakaongeza bao la pili dakika ya 65 kwa mkwaju wa penati uliofungwa na Jumanne Elfadhili kabla ya Mohamed Rashidi kukamilisha ushindi wa magoli 3-1 kwa kufunga bao dakika ya 87 huku Babu Ally akiifungia Mbeya City bao la pili dakika ya 90.
Rekodi hiyo mbovu ya Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons, inamfanya kocha Juma Mwambusi kuwa kocha pekee aliyewahi kuifundisha Mbeya City na kupata ushindi dhidi ya ‘wajelajela’ wa Mbeya katika mechi za ligi.
Matokeo ya Mbeya City na Tanzania Prison katika mechi 9 zilizopita
2013/14
- Tanzania Prisons 0-2 Mbeya City
- Mbeya City 1-0 Tanzania Prisons
- Mbeya City 2-2 Tanzania Prisons
- Tanzania Prisons 1-0 Mbeya City
- Tanzania Prisons 1-0 Mbeya City
- Mbeya City 0-0Tanzania Prisons
- Mbeya City 0-0 Tanzania Prisons
- Tanzania Prisons 2-0 Mbeya City
- Tanzania Prisons 3-1 Mbeya City
- Mbeya City ?? Tanzania Prisons
0 comments:
Post a Comment