REFA
Mfaransa, Tony Chapron usiku wa jana amefanya kituko cha aina yake
baada ya kumpiga teke beki wa Nantes, Diego Carlos kabla ya kumuonyesha
kadi ya pili ya njano na kumtoa kwa nyekundu dakika ya 90 na ushei timu
yake ikifungwa 1-0 na Paris Saint-Germain katika mechi ya Ligue 1 Uwanja wa Beaujoire - Louis Fonteneau mjini Nantes.
Carlos alikuwa tayari ana kadi ya njano wakati Paris Saint-Germain wanapeleka
shambulizi la kujibu na mchezaji huyo Mbrazil mwenye umri wa miaka 24
akagongana na refa huyo wakati anakimbia kurudi kuihami timu yake
isifungwe.
Refa
alikuwa anakimbia na mchezo na bahati mbaya akapamiana na Mbrazil huyo
na kuanguka chini, lakini ajabu akainuka na kumrudishia kwa teke kabla
ya kumuonyesha kadi mfululizo.
Refa Tony Chapron akimuonyesha kadi nyekundu, beki wa Nantes, Diego Carlos jana
Beki
wa Nantes alionyesha uungwana kwa kumsaidia refa Chapron baada ya
kuanguka, ingawa hiyo haikumsaidia kumuepusha na kadi na akawapa mpira
wa adhabu PSG wapige.
PSG iliibuka na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo huo, bao pekee la winga Muargentina, Angel Di Maria dakika ya 12.
Rais wa Nantes, Waldemar Kita ametaka refa Chapron afungiwe miezi sita.
"Nimepokea SMS 20 duniani kote zikiniambia huyu refa ni wa ovyo,"alisema Kita akizungumza na L'Equipe.
0 comments:
Post a Comment