HISTORIA ya kusisimua ya maisha ya Lionel Messi kutoka Argentina hadi Barcelona imesimuliwa kwenye pea ya kiatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amepatiwa zawadi ya kiatu na msanii wa Paraguay kilichobeba historia ya maisha yake.
Lili
Cantero amekuwa akivutiwa mno na maisha ya Messi na mafanikio yake
kiasi kwamba akaamua kuchukua muda wake kubuni zawadi nzuri ya kumpa.
Kiatu
hicho kimepambwa na picha za kuanzia Messi yuko mdogo Amerika Kusini,
picha za familia yake akiwa na mkewe, Antonella Roccuzzo na amewashika
watoto wake, Thiago na Mateo.
Msanii
huyo ameelezea zaidi kuhusu viatu hivyo akisema kwamba hayo ni matokeo
ya kazi ngumu anayoifanya Messi inavyomlipa. "Viatu hivyo vilipelekwa
Barcelona kama zawadi kwa mchezaji huyo, kikiwa kimechorwa chote,".
"Kiatu
hicho kinazungumzia maisha ya Messi, kikiwa kimepambwa kwa picha za
historia yakena namna alivyojituma kufikia mafanikio,".
Kutoka Paraguay na upendo Love, kwa dunia.
Messi si mwanasoka wa kwanza kukabidhiwa viatu vilivyochirwa hivyo kutoka kwa msanii huyo mwenyeb kipaji.
Mwanasoka wa kimataifa wa Paraguay, Derlis Gonzalez wa klabu ya Dynamo Kiev pia ni miongoni mwa wachezaji wengine waliowahi kupewa zawadi hiyo.
0 comments:
Post a Comment