KIUNGO Henrikh Mkhitaryan anatarajiwa kujiunga na Arsenal kutoka Manchester United licha ya onyo kutoka kwa wakala wake kwamba anaweza kuvuruga usajili wa Alexis Sanchez kwenda Old Trafford.
Uhamisho
wa Mkhitaryan kwenda Emirates unakaribia baada ya kugundulika United
wameipiku Manchester City katika mbio za kuwania saini ya Sanchez kutoka
Arsenal.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Armenia mkataba wake Old Trafford unamalizika
mwaka 2020 na wakala wake, Mino Raiola amesema anaweza kuondoka kwa
vipengele vyake binafasi au kubadilishwa na Sanchez.
Pamoja
na hayo inafahamika kwamba Mkhitaryan amekubali hana maisha zaidi
United na sasa anatarajia majadiliano ya kuongeza mshahara wake kutoka
Pauni 140,000 kwa wiki anazolipwa sasa.
Kiungo wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan anatarajiwa kujiunga na Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Raiola,
ambaye aliingiza Pauni Milioni 41 katika mauzo ya Paul Pogba ya Pauni
Milioni 89 kwenda United kutoka Juventus na pia alimuwakilisha Zlatan
Ibrahimovic, pia anaweza kuwa sehemu ya dili hili.
Arsenal
wanataka Pauni Milioni 35 kumuuza Sanchez ambaye atakuwa anapata
mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki United pamoja na Pauni Milioni 20 za
kusaini mkataba na Pauni Milioni 15 atakazolipwa wakala wake, Fernando
Felicevich.
Mkhitaryan
alijiunga na United kwa dau la Pauni Milioni 26 kutoka Borussia
Dortmund mwaka 2016 na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ya 28
hakujumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichomenyana na Stoke City
usiku wa Jumatatu huku kocha Jose Mourinho akiweka wazi kwamba hana
nafasi kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment