Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema, ndani ya siku mbili za mapumziko kabla ya mechi yao ya nusu fainali watakuwa wakijiandaa kwa ajili ya mchezo huo ili kuhakikisha wanashinda.
“URA ni timu nzuri na wamewafunga Azam na Simba timu ambazo ni nzuri, tumeshawaona wanavyocheza tuna siku mbili hizi za mapumziko tutajipanga na kujiandaa jinsi gani tuingie.”
Mechi za nusu fainali ya Mapinduzi Cup zitachezwa Jumatano Januari 10, 2018 ambapo timu mbili zitakazoshinda mechi za nusu fainali zitacheza fainali ya Mapinduzi Cup 2017/18.
0 comments:
Post a Comment