Nyota
wa zamani wa Manchester United, Angel di Maria akishangilia baada ya
kuifungia mabao matatu peke yake Paris Saint-Germain dakika za kwanza,
58 na 62 katika ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Sochaux kwenye
mchezo wa marudiano wa Robo Fainali Kombe la Ufaransa usiku wa jana
Uwanja wa Auguste-Bonal mjini Montbeliard. Bao lingine la PSG lilifungwa
na Edinson Cavani dakika ya 27 wakati la Sochaux lilifungwa na
Florian Martin dakika ya 13.
Katika mchezo huo, kipa wa PSG, Kevin Trapp alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 wakati wamekwishamaliza idadi ya wachezaji wa kubadili, ikabidi Dani Alves akasimame langoni kumalizia dakika za majeruhi

0 comments:
Post a Comment