Klabu ya Simba yaibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Azam FC mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.
Bao la Simba SC likifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi kunako dakika ya 37 kipindi cha kwanza.
Kwa matokeo hayo Simba SC inaongoza katika msimamo wa ligi kwa kuwa na jumla ya pointi 41 na kuweka rekodi ya kutopoteza hata mchezo mmoja mpaka sasa nafasi ya pili ikishikiliwa na Yanga SC wenye alama 33.
0 comments:
Post a Comment