Tuesday, February 20, 2018

Luis Enrique yupo katika nafasi nzuri ya kumrithi Antonio Conte kwenye nafasi ya kocha mkuu Chelsea baada ya kuibuka ripoti kuwa bodi ya timu hiyo imeanza mchakato wa kusaka kocha mpya.

Inadaiwa Chelsea imeanza mazungumzo na kocha huyo wa zamani wa Barcelona baada ya kujiridhisha kuwa Antonio Conte anaipeleka timu kubaya.

Kibarua cha Conte kimezidi kuingia hatarini baada ya kichapo cha 4-1 kutoka kwa Watford Jumatatu usiku, siku chache baada ya kunyukwa 3-0 na Bournemouth.

0 comments:

Post a Comment