Yanga wamelazimika kusubiri kwa zaidi ya dakika 40 uwanjani baada ya
kumaliza mazoezi yao jioni hii kutokana na kucheleweshewa basi
wanalolitumia kwa safari zao tangu walipofika Shelisheli.
Mazoezi hayo ya saa mbili yalianza mnamo saa 9 alasiri na kumalizika saa
11 jioni kwa muda wa huku, lakini yalipomalizika walijikuta solemba
baada ya basi hilo kutoonekana uwanjani hapo.
Kutokana na kuchelewa kwa basi hilo, viongozi wa Yanga, Samuel Lukumay
na Hussein Nyika kwa kushirikiana na mwakilishi wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Issah Bukuku walijitahidi kuwasiliana na
uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) ili
kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo hilo.
Uongozi huo wa SFF waliitaka Yanga kuwa na subira huku wakiambiwa kwamba basi liko jirani na uwanjani hapo linakuja.
Hata hivyo Yanga walilazimika kusubiri kwa zaidi ya dakika 40 ndipo
likaja basi lingine ambalo lilikuwa tofauti na lile la mwanzoni.
Maelezo waliyopewa ni kwamba basi la awali lilishindwa kufika uwanjani
hapo kutokana na kupata hitilafu wakati lilipokuwa linakwenda kuwafuata.
0 comments:
Post a Comment