
West Ham
imemsimamisha kazi mkurugenzi wa usajili wa wachezaji Tony Henry kuhusu
madai kwamba klabu hiyo haitawasajili teza wachezaji zaidi wa Afrika.
Gazeti la Daily Mail liliripoti kwamba Henry alisema kuwa wachezaji wa Afrika huzua fujo wasiposhirikishwa katika mechi Katika taarifa, West Ham imesema kuwa haitavumilia ubaguzi wa aina yoyote ule na hivyobasi imemchukulia hatua mkurugenzi huyo kutokana na hatari ya madai yake.
Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limesema kuwa litachunguza rasmi swala hilo.
- West Ham yakataa tena kumuuza Payet
- Mchezaji akataa kuheshimu wimbo wa taifa Marekani
- Balotelli abaguliwa nchini Ufaransa
''klabu hiyo haitatoa tamko jingine lolote hadi pale uchunguzi utakapokamilika. Wafanyikazi wote hufunzwa kuhusu usawa na kutokuwa na upendeleo'', ilisema klabu hiyo.
Shirikisho la soka nchini Uingereza limesema kuwa lilishangazwa na matamshi hayo na kufurahia hatua iliochukuliwa na West Ham.
''Shirikisho la soka la Uingereza linashutumu maono kama hayo na hayataruhusiwa katika soka'', alisema.
0 comments:
Post a Comment