Yaliyotokea usiku wa jana katika siku ya mwisho ya usajili
Wakati jana Tottenham wakiiua Manchester United Lucas Moura naye amejiunga na Tottenham Hotspur kwa ada ya uhamisho wa £25m, Moura amesaini kuitumikia Tottanham hadi mwaka 2023.
Olivier Giroud jana alikuwepo uwanjani wakati timu yake mpya ya Chelsea ikifungwa bao 3 kwa nunge na Giroud amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu wa kuitumikia Chelsea.
Mlinzi Jon Flanangan wa Liverpool naye amejiunga na klabu ya Bolton kwa mkopo na sasa Flanangan ataitumikia Bolton Wanderes hadi mwisho wa msimu huu.
Swansea City nao wamefanikiwa kumrudisha Andre Ayew kwa ada ya £18m kutoka West Ham na sasa huo ndio utakuwa usajili ghali zaidi katika klabu ya Swansea kwa sasa.
Kinda aliyekuwa akitabiriwa kufanya makubwa na klabu ya Everton Ademola Lookman amepelekwa RB Leizpg kwa mkopo na sasa atakaa Bundesliga hadi mwisho wa msimu.
Islam Slimani amefanikiwa kujiunga na klabu ya Newcastle United kwa mkopo, Slimani aliyekuwa hana namba ya uhakika Leicester City sasa atabaki Newcastle hadi mwisho wa msimu.
Eliaquim Mangala naye baada ya kupata wakati mgumu kuanza katika kikosi cha Manchester City sasa beki huyo amejiunga na klabu ya Everton kwa mkopo.
Lakini klabu ya Leicester City imesema haikujua jana Ryad Mahrez alikuwa wapi lakinj wamefanikiwa kuzima jaribio la Manchester City kutaka kumnunua Mualgeria huyo
0 comments:
Post a Comment