“Nimeongea na Messi baada ya mchezo kumalizika, amesema anajiona mtu mwenye furaha zaidi kwa siku ya leo kwani mbali ya kupata mtoto lakini amefurahishwa zaidi na matokeo. Napenda kusema kuwa ushindi huu ni zawadi yake, hakuna zawadi nyingine kubwa kwa mchezaji wa Barcelona zaidi ya ushindi,“amesema Ernesto Valverde.
Mabao ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez dakika ya 15, na Philippe Coutinho, dakika ya 28 na kuifanya klabu hiyo kujikita kileleni kwa alama 72.
0 comments:
Post a Comment