Messi apata mtoto wa tatu, amfukuzia Ronaldo kimya kimya
Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi na mkewe Antonella Roccuzzo wamefanikiwa kupata mtoto wao wa tatu wa kiume.
Hilo amethibitisha Messi kupiia mtandao ake w Instagram kwa kuweka picha hiyo hapo chini na kuandika, “Karibu Ciro! Asante Mungu kila kitu kilikwenda kikamilifu. Mama na mtoto wote wapo salama. Tunafuraha kubwa sana!!!!! .”
Mtoto huyo tayari amepewa jna la Ciro ambapo anaungana na kaka zake wawili akiwemo Mateo (2) na Thiago (5).
Wakati huo huo mpinzani wa Messi, Cristiano Ronaldo ana watoto wanne, wakiwemo wwili mapacha.
kutokana na ujio wa mtoto huyo Messi amepewa mapumziko na timu yake hivyo hatakuwepo katika mchezo wa usiku wa leo ambao Barcelona watacheza na Malaga katika mechi ya La Liga na nafasi yake imepangwa kuchukuliwa na mchezaji Yerry Mina.
0 comments:
Post a Comment