WACHEZAJI
wa Yanga wamewaomba wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa
wingi leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam ili kuwapa hamasa washinde
mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United.
Kipa Ramadhani Kabwili, beki Juma Abdula na kiungo Juma Mahadhi ndiyo wametumika katika video fupi ya youtube kufikisha ujumbe wa wachezaji wenzao kwa wapenzi wa timu.
Mkongwe Juma Abdul amesema kwamba ni muhimu mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani, kwani hiyo itawapa hamasa wapigane na kushinda leo.
Kutoka kulia Juma Mahadhi, Juma Abdul, Geoffrey Mwashiuya na Youthe Rostand wanawaita mashabiki wao Taifa leo
Kipa chipukizi Kabwili yeye amesema kwamba mashabiki wa Yanga hawapaswi kujiweka nyuma, wanatakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwapa sapoti wachezaji wao na akasema wao watapigana washinde mchezo wa leo.
Kwa, upande wake, Juma Mahadhi amesema kwamba ushindi leo ni muhimu na zaidi malengo yao ni ubingwa wa Ligi Kuu, hivyo amewaomba wapenzi wa Yanga wajitokeze uwanjani kwa wingi leo.
Yanga wanawakaribisha Stand United jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakihitaji ushindi ili kurudi nafasi ya pili, kufuatia Azam FC kushinda 2-1 dhidi ya Mbao FC jana.
Ushindi wa jana unaifanya Azam FC ifikishe pointi pointi 44, sasa ikiizidi Yanga pointi moja huku ikizidiwa pointi mbili na Simba iliyo kileleni kwa pointi 46, ingawa yenyewe imecheza mechi mbili zaidi.

0 comments:
Post a Comment