WAKALA wa Mario Balotelli, Mino Raiola amekasirishwa na kitendo cha mshambuliaji huyo kuachwa kwenye kikosi cha sasa cha Italia licha ya kuwa katika kiwango kizuri.
Balotelli
amefunga mabao 22 katika mechi 31 alizoichezea klabu yake, Nice katika
Ligue 1 nchini Ufaransa msimu huu, lakini kocha wa muda wa Italia, Luigi
Di Biagio hajamjumuisha kwenye kikosi kitakachomenyana na Argentina na
England.
Raiola, ambaye pia anamuwakilisha mchezaji ghali wa Manchester United, Paul Pogba, amesema hajafurahishwa na uamuzi wa kumuacha Balotelli kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Argentina na England.
Mario Balotelli has been left out of the most recent Italy squad by Luigi Di Biagio PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Tumesikitishwa
na kutoitwa kwa Balotelli,"amesema Raiola. Tumesikitishwa pia na
ufafanuzi tulioupokea, hadharani kwa sababu hatujazungumza na mtu hata
mmoja,".
Mshambuliaji
huyo ameachwa baada ya kuitwa kwa wachezaji wapya kabisa The Azzuri,
Patrick Cutrone na Federico Chiesa hawajaichezea hata mechi moja
Italia.
Raiola amesema kwa rekodi yake msimu huu, Balotelli anastahili kuwemo kikosini kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014.
"Kama
Di Biagio anasema idadi (ya mabao) haihesabiwi kwa mshambuliaji, kisha
milango ya timu ya taifa imefungwa kwa mchezaji kama yeye. Tatizo si
kocha - ni mfumo wa soka. Tuna shirikisho linalofanya kazi bila
mipango,"amesema.
"Timu ya taifa lazima iwakilishwe na wachezaji bora, hivyo kama wachezaji wazuri hawaendi, basi hatujui vigezo,"ameongez
0 comments:
Post a Comment