Tuesday, March 20, 2018

Mohammed Salah ananyatiwa na barcelona, Real Madrid na PSG



Barcelona, Paris St-Germain na Real Madrid zinataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah , 25 kwa dau la uhamisho litakalovunja rekodi la £200m. Raia huyo wa Misri amefunga mabao 28 katika ligi ya Uingereza msimu huu. (Sun)
Beki wa Manchester United Luke Shaw, 22, anahisi kwamba meneja Jose Mourinho anamnyanyasa na kwamba raia huyo wa Uingereza huenda akawasilisha malalamishi yake kwa naibu afisa mkuu mtendaji katika klabu hiyo Ed Woodward. (Mirror)
Luke Shaw na Mourinho
Mourinho anapanga kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27, katika klabu ya Manchester United. (Star)
Beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin
United tayari imemuulizia beki wa Arsenal Hector Bellerin, lakini Juventus wanapigiwa upatu kumsajili mchezaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 23. (Mirror)
Pendekezo la mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko kuhamia Chelsea mwezi Januari liligonga mwamba baada ya Roma kujiondoa katika mkataba huo wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32.(Radio Rai, via Metro)
Mkufunzi wa klabu ya Bayern Munich Jupp Heynckes amepinga usajili wa mshambuliaji wa Bordeaux Malcom, 21. Raia huyo wa Brazilian amehusishwa na uhamisho wa Tottenham na Arsenal. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino anasema kuwa Liverpool ililazimika kubadilisha mtindo wa mchezo wake kufuatia uhaimsho wa mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho aliyehamia Barcelona. (Goal)
Mwandishi wa New York Times Rory Smith anaamini Firmino ataipatia hamu Bayern Munich kumsajili iwapo mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Poland Robert Lewandowski, 29, ataondoka mwisho wa msimu huu . (BBC Radio 5 live)
Utafiti wa uhamisho unadai kwamba mshambuliaji wa Tottenham nchini Uingereza Harry Kane ataipatia faida kubwa Tottenham zaidi ya Lionel Messi kwa Barcelona.. (Express)
Beki wa Chelsea Andreas Christensen aliomba ushauri kwa nahodha wa zamani wa klabu hiyo John Terry - anayechezea Aston Villa - baada ya kiwango chake cha mchezo kudorora. (Eurosport Denmark, via Evening Standard)
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amefichua kwamba hatapiki tena wakati wa mechi kwa sababu hatumii tena chokoleti na vinywaji vyenye gesi. (Goal)
Mshambuliaji wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo aliwahakikishia wenzake wa Real Madrid kwamba atashinda taji la mfungaji mwenye mabao mengi katika ligi ya La Liga licha ya Messi kuwa na mabao 11 zaidi ya yake. (Marca)
Brazil itatumia uwanja wa mazoezi wa Tottenham kuajiandaa katika kombe la dunia la Urusi mwisho mwa msimu huu. (Evening Standard)

0 comments:

Post a Comment