Tuesday, March 20, 2018



Kwa mujibu wa jarida la 'The Sun' limeripoti kuwa Mshambuliaji wa Liverpool aliye katika fomu hivi sasa, Mmisri, Mohamed Salah, anawaniwa na timu tofauti za Ulaya.

PSG, Real Madrid na FC. Barcelona ndiyo klabu zinazonyatia saini ya mchezaji huyo ili kuweza kumsajili.

Dau la £200m litakalovunja rekodi ya uhamisho, ndiyo linatajwa kuwa linaweza kumng'oa mchezaji huyo kutoka Liverpool.

Salah ameifungia Liverpool jumla ya mabao 28 katika msimu huu wa Ligi Kuu England.

0 comments:

Post a Comment