Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amesema kuwa Paul Pogba hatoweza kuwa na furaha kwenye kikosi cha Manchester United.
Paul Pogba yuko kwenye kikosi cha Ufaransa kitakachokuwa kinacheza michezo ya kirafiki dhidi ya Colombia na Russia.
"Nina uhakika nitajua mengi kutoka kwake, lakini kwa namna hali ilivyo hatoweza kuwa na furaha".
"Sijui kwanini, lakini inawezekana kukawa na sababu mbalimbali" alisema Deschamps.
Pogba alikosekana kikosini kwenye mchezo uliopita Manchester United walipocheza dhidi ya Brighton FC.
Wakati huohuo United itakuwa itakuwa ina kibarua kingine dhidi ya Swansea City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, Machi 31 2018.
0 comments:
Post a Comment