SHIRIKISHO
la Soka la Kimataifa (FIFA) limemfungia kwa miezi sita kutocheza soka
mshambuliaji wa Singida United, Danny Lyanga kwa kosa la kusaini timu
mbili kwa msimu mmoja, nyingine Fanja SC ya Oman.
Lyanga amesajiliwa Singida kipindi cha usajili wa dirisha dogo akitokea katika klabu ya Fanja FC ya Oman, hali ya kuwa akiwa ndani ya mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo kutoka nchini ya Kiarabu.
Mshambuliaji huyo tangu amesajiliwa ndani ya timu hiyo alicheza michuano ya kombe la Mapinduzi mwanzoni mwa mwaka huu, hajacheza mechi hata mmoja ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Danny Lyanga (katikati) amefungiwa kwa kosa la kusaini timu mbili kwa msimu mmoja, Singida United na Fanja SC ya Oman
Taarifa za uhakika zilizoifikia Bin Zubeiry Sports - Online kutoka katika klabu ya Fanja, kwamba Lyanga aliondoka katika klabu hiyo baada ya kutakiwa kujiunga na timu ya Taifa ya Tanzania katika michuano ya Challenji mwaka jana.
Alisema wakati Lyanga anajiunga na timu ya Taifa akiwa ameshasaini mkataba wa miaka miwili kutumia Fanja, pia alipofika huko na kusaini mkataba na Singida bila ya kuzungumza na uongozi wa timu yake ya zamani.
“Lyanga hachezi ligi hadi msimu ujao, kwani Fifa wamemfungia miezi sita, kwa kitendo cha kusaini mkataba na timu nyingine hali ya kuwa akiwa ndani ya mkataba”, alisema.
Mtoa habari huyo alisema kitendo cha straika huyo kupeleka malalamiko yake Fifa kuwashtaki Fanja, ikapeleka udhibiti wa mkataba waliongia na mchezaji huyo na kesi kugeuka kwake kwa maamuzi ya kumfingia.
Alipotafutwa Lyanga, hakutana kuzungumzia suala hilo na kudai kwamba yupo Bangamoyo na suala hilo atafutwe Katibu wa Singida atazungumzia.

0 comments:
Post a Comment