Friday, March 23, 2018


Wakati tumebakiza siku 83 kabla ya kuanza kwa Kombe la dunia – timu za taifa zimeanza kujiandaa na michuano hiyo kwa mechi za kirafiki ambazo hupaswi kuzikosa…
Uruguay vs Czech Republic, Friday, March 23rd, saa 8:35 mchana

Uruguay siku zote ni washindani na safari hii wanakutana na timu ambayo haiendi World Cup. Luis Suarez anaungana na Cavani kutengeneza safu ya ushambuliaji dhidi ya Czech!
Russia vs Brazil, Friday, March 23rd, saa 1 usiku

Wenyeji wa michuano wanakutana na mabingwa wa kihistoria wa Kombe la dunia katika mchezo wa kirafiki kesho. Mchezo huu utapigwa katika dimba la Luzhniki. Brazil watacheza bila Neymar mwenye majeruhi – na watakuwa na mtihani wa kutetea rekodi yao ya kutofungwa chini Tite.
.
Portugal vs Egypt, Friday, March 23rd, saa 4 usiku.

Huu ni mchezo ambao unawakutanisha washambuliaji walio kwenye form kuliko wote barani ulaya, Mohamed Salah ambaye anaongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha ulaya dhidi ya Cristiano Ronaldo ambaye amefunga magoli 21 katika mechi 11 zilizopita.
Peru vs Croatia, Friday, March 23rd, 4:30 usiku

Nafasi ya kuziona timu mbili ambazo hazipewi nafasi kubwa ya kubeba taji nchini Russia. Wacroatia dhidi ya Peru – mchezo utakuwa na ufundi mkubwa kutoka kwa wachezaji kama Modric, Rakitic, Farfan,, Cueva, na wengineo!
Serbia vs Morrocco, Friday, March 23rd, 4:30 usiku
Macho ya nawakala wengi wa soka yatakuwa kwenye mchezo huu – mmoja ya wachezaji wanaotarajiwa kuwa na soko kubwa kwenye dirisha la usajili Milinkovic-Savic ataungana na Akina Nemanja Matic kuumana na Simba wa Afrika ya Kaskazini – Morrocco
Germany vs Spain, Friday, March 23rd, 4:45 usiku

Timu za mwisho kubeba taji la dunia wanakutana kupimana misuli kabla ya kwenda Russia. Mchezo unategemewa kuwa na ufundi mkubwa – utakaokuwa wazi bila kupaki mabasi. Ni mchezo ambao utakupa ladha kamili ya michuano mikubwa – ikihusisha wachezaji bora kabisa duniani – kuanzia magolikipa, mabeki, viungo mpaka washambuliaji.
Holland vs England, Friday, March 23rd, saa 4:45 usiku.

Kwa bahati mbaya Uholanzi hawatokuwa miongoni mwa timu zitakazopanda ndege kwenda Russia mwaka huu lakini watakuwa kipimo sahihi cha Uingereza, hata hivyo Waingereza watamkosa Harry Kane!
Italy vs Argentina, Friday, March 23rd, saa 4:45

Italia ni miongoni mwa mataifa makubwa ambayo hatutowaona Russia- hata hivyo mchezo wa Italy vs Argentina ni mchezo wenye hadhi ya fainali ya kombe la dunia. Italy wanajipanga upya huku kocha wa Argentina akiwa bado anaisaka first eleven kwa ajili ya World Cup! Lakini pia huenda tukapata nafasi ya kushuhudia tena Messi akiumana na Buffon.
France vs Colombia, Friday, March 23rd, 5 usiku

Mechi iliyojaa vipaji kutoka barani ulaya na Amerika ya kusini! Griezmann, Mbappe, Pogba, James Rodriguez, Falcao na Muriel. Wanaume hawa wote wapo Russia – Ufaransa wakiwa ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri nchini Urusi mwaka huu, Colombia wakiwa nao wanataka kuvuka walipoishia 2014.
Iceland vs Mexico, Friday, March 23rd, saa 6 usiku

Baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Euro 2016, na kisha kufanikiwa kufuzu kucheza kombe la dunia kwa mara ya kwanza – Iceland sasa wapo tayari kwenda Russia kufanya majaabu – lakini kwanza ni kuanza vizuri michezo ya maandalizi kwa kuanzia na Mexico ambao kombe la dunia wana uzoefu nalo.

0 comments:

Post a Comment