KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba ambaye kwa sasa hafanyi vizuri ameelezea kiu yake ya kutaka siku moja kucheza na mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Neymar.
Nyota
huyo wa United amesema kwamba wakati wa makuzi yake alikuwa anampenda
mchezaji wa zamani wa kimataifa wa England, Chris Waddle.
Pogba, kwa sasa yuko na timu yake ya taifa, Ufaransa inayojiandaa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Colombia Ijumaa.
Na katika mahojiano na chaneli ya Televisheni ya Argentina, TyC Sports alionyeshwa kipande cha nukuu ya Neymar akisema: "Napenda namna alivyo na wakati fulani tunaenda kucheza pamoja,".
Pogba
akajibu kwa kusema: "Ndiyo, Neymar, Neymar. nampenda pia. Pia ana maana
ya furaha uwanjani. Kwa Brazil, soka ni kila kitu, ni maisha ya Brazil.
Kila mmoja anacheza soka.
"Napenda
kumuona uwanjani anacheza, kwa ujuzi na ufundi wake. Ni staili tofauti.
Unaposema neno Neymar duniani, kila mmoja anafahamu huyo ni nani na
anafanya nini. Pamoja na hayo kama nitacheza naye siku moja itakuwa
safi,"'
Wakati
huo huo, mchezaji huyo wa zamani wa Juventus amesema wakati anaibuka
kisoka alikuwa anawapenda wachezaji kama Zinadine Zdane, Lionel Messi,
Ronaldinho Gaucho na Ronaldo Lima.
Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesema anapenda siku moja kucheza pamoja na Neymar PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Nilikuwa
nina videos za Maradona. Pele, Chris Waddle, Kaka, wachezaji wengi.
Nilitaka kuwa na vitu vua wachezaji wote hao nyota,".
Kwa
sasa Pogba hana wakati mzuri sana Old Trafford na kocha, Jose Mourinho
amemkuwa akimtema Mfaransa huyo kwenye mechi kadhaa muhimu.
Anatarajiwa kutumia michezo hii ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Colombia na Urusi kurejesha hali yake ya kujiamini.
0 comments:
Post a Comment