Monday, March 19, 2018


WINGA Simon Msuva atakuwa mchezaji mwingine wa Tanzania baada ya Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na klabu zisizo za Tanzania.
Hiyo ni baada ya timu yake, Difaa Hassan El Jadida kulazimisha sare ya 2-2 na wenyeji, AS Vita Uwanja wa The Martyrs de la Pentecote mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa matokeo hayo, DHJ inakwenda hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza siku 11 zilizopita Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan, tena bao pekee la Msuva.
Msuva ambaye hakuanza kwenye mchezo wa leo mjini Kinshasa, amefunga mabao manne hadi sasa kwenye michuano hiyo, kufuatia kufunga hat-trick katika mchezo wa Raundi ya Awali dhidi ya Benfica Bissau ya Guinea Bissau.
Simon Msuva (katikati) mbele kabla ya mchezo wa kwanza na AS Vita mjini Jadida wiki iliyopita

Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji kwa sasa na Ulimwengu ambaye ni mchezaji huru walicheza na kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa na TP Mazembe ya DRC.
Msuva amewahi kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho tu mwaka juzi akiwa na klabu yake iliyomuinua kisoka hadi akaoneksana Morocco, Yanga SC.
Kikosi cha Difaa Hassan El Jadida kilichoanza leo mjini Kinshasa

0 comments:

Post a Comment