Davide Astori aliyekuwa na umri wa miaka 31 alifariki akiwa uzingizini, wachezaji wenzake waligundua hilo na kwenda kuvunja chumba chake cha hotel, baada ya Davide Astori kutotokea wakati wa kupata kifungua kinywa ndio wakaanza kujiuliza shida ni nini?
Staa huyo aliyewahi kuchezea vilabu mbalimbali ikiwemo AC Milan, mastaa wenzake leo walijumuika katika kanisa la Santa Croce mjini Florence kwa ajili ya kumuaga, inaaminika kuwa Davide Astori mauti yalimkuta kutokana na shambulio la moyo la ghafla.
Baada ya msimba huo ambao umeacha pengo kwa familia ya Davide Astori aliyeacha mke na mtoto wa kike mmoja, uongozi wa club ya Fiorentina wameamua kumlipa mshahara kwa maisha yote mke wa Davide Astori ili aweze kujikimu kimaisha na kumuhudumia mtoto wake.
0 comments:
Post a Comment