Asubuhi ya Jumanne nilionya mashabiki wote walioamini PSG wanaweza kupindua matokeo ya mchezo wa kwanza wasiwaze jambo hilo, na hilo ndilo limetokea baada ya PSG kupewa kili nilichotarajia.
Nani mwingine kama sio CR7? Mreno huyo amefunga bao lake la 12 la Champions League na sasa amesawazisha idadi ya mabao na yale ya msimh uliopita ya Champions League ambapo alifunga 12.
Hii ni mechi ya 9 mfululizo kwa CR7 kufunga katika mechi za Champions League, bao lingine la Real Madrid lilifungwa na Casemiro huku lile la kufutia machozi la PSG likifungwa na Edinson Cavanni.
PSG walimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya Marco Veratti kuoneshwa kadi nyekundu, na aggrgate ya mabao 2 kwa 5 inawafanya Madrid kucheza robo fainali ya 8 mfululizo.
Sare ya bila kufungana nayo imewapeleka Liverpool robo fainali huku golikipa wa Fc Porto Iker Casillas akiweka rekodi katika mchezo huo kwa kuwa kipa wa kwanza kucheza na Liverpool katika Champions League msimu huu bila wavu wake kuguswa.
0 comments:
Post a Comment