Thursday, March 8, 2018

Winga wa Manchester City, Leroy Sane akimtoka mchezaji wa FC Basle, Fabian Frei katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Etihad. Basle ilishinda 2-1, mabao yake yakifungwa na Mohamed Elyounoussi dakika ya 17 na Michael Lang dakika ya 71, baada ya Gabriel Jesus kutangulia kuifungia Man City dakika ya nane ambayo inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2, kufuatia awali kushinda 4-0 Basle

0 comments:

Post a Comment