IMERIPOTIWA Real Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski msimu ujao.
Robert Lewandowskin amefikia makubaliano ya kuhamia Real Madrid msimu ujao PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo,
mwanasoka huyo wa kimataifa wa Poland amefikia makubaliano ya vipengele
binafsi kwa mkataba wa miaka miwili na Madrid baada ya mikutano kadhaa
mwezi huu.
Rais
wa Madrid, Florentino Perez ameamua kumchukua mshambuliaji huyo wa
Bayern huku akisikilizia mpango wa kumsajili Neymar kutoka Paris Saint-Germain.
Real
imekuwa ikimtaka Lewandowski kwa muda fulani na imefanikiwa kupambana
na Chelsea, PSG na Arsenal kuzungumza kwanza na wawakilishi wa mchezaji
huyo na inafahamika mshambuliaji huyo anapenda zaidi kuhamia Bernabeu.
Robert Lewandowskin amefikia makubaliano ya kuhamia Real Madrid msimu ujao PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Madrid
pia imekuwa na dhamira ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Harry
Kane, lakini haina matumaini ya kuipata saini ya mchezaji huyo kufuatia
Mwenyekiti, Daniel Levy kukataa mazungumzo.
Jambo
hilo moja kwa moja limegeuza nia ya Perez na kuhamia kwa Lewandowski,
ambaye ana rekodi nzuri na amefunga mabao 32 Bundesliga msimu huu.
Anaaminika
kuwa mbadala sahihi wa mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema, ambaye
amekuwa na msimu mbaya akifunga mabao saba tu katika mechi 31.
Madrid
pia inamtaka winga wa Chelsea, Eden Hazard imhamishie Hispania, kwani
Mbelgiji huyo yupo katika miezi 15 ya mwisho ya mkataba wake na bado
hajasaini mkataba mpya.
Hazard
inafahamika bado anasikilizia kama Chelsea itafuzu kucheza Ligi ya
Mabingwa Ulaya msimu ujao ndiyo asaini mkataba mpya, vinginevyo atakuwa
tayari kuondoka.
Inategemea
na mchezaji atakayesajiliwa na Real Madrid juu ya kufungua njia kwa
Gareth Bale, ambaye anatakiwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England
kuondoka.
0 comments:
Post a Comment