Wednesday, March 21, 2018



Kikosi cha Simba kinataraji kuanza mazoezi ya kujiwinda na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara Jumamosi ya wiki hii.

Simba itaanza kujiandaa kuelekea mchezo na Njombe Mji FC ya mjini Njombe Ijumaa hii kufuatia wachezaji wake kupewa mapumziko ya siku kuanzia Jumanne ya wiki hii.

Kikosi hicho kitakuwa ugenini kucheza mechi hiyo ya ligi Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba.

Baada ya mechi hiyo, Simba itakuwa inajiandaa tena kukabiliana na walima miwa wa Mtibwa, Mtibwa Sugar.

Kikosi hicho kimewasili nchini Jumatatu baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa suluhu ya 0-0 ugenini na sare ya 2-2 hapa nyumbani.

0 comments:

Post a Comment